Ni safari ya matumaini iliyotangazwa na waziri mkuu aliyejiondoa madarakani kwa ile kashfa ya RICHMOND mwaka 2008 ambapo wengi walihusishwa lakini yeye kwa busara zake aliamua kuachia ngazi kama ishara ya uwajibakaji.
Wakati Tanzania inahitaji kiongozi bora atakaye weza kulipeleka taifa letu katika hatua ambayo haijawahi kutokea tangu tulipopata uhuru, wanachama wa vyama vya siasa nchini wameanza kutangaza nia zao na kumwaga sera zao zenye malengo chanya kwa taifa hili tajiri lakini masikini kuliko.

Wameanza wagombea kutoka chama cha mapinduzi na sera zao zenye malengo ya kuleta maendeleo chanya kwa taifa hili kitu ambacho mwandishi ametathimini na kuona kwamba watu hawa huenda ni walaghai tu kwa sababu wanazungumzia matatizo amabayo wangeyatatua wakati wa uongozi wao serikalini.

Ni mawaziri waliopita na wameshindwa kutekeleza hata moja ya walioyataja katika sera zao ikiwa ni pamoja na rushwa, ufisadi, umaskini,elimu duni, usawa afya na amani , je wataweza wakipewa nafasi ? kama wataweza walikuwa wapi muda wote huo? je walikuwa wanamkomoa rais aliye madarakani Jakaya Kikwete? hapana shaka tukisema hawana jipya la kutueleza watanzania.

Hatuwezi kusahau RICHMOND,KAMPENI TOKOMEZA UJANGILI na TEGETA ESCROW haya ni baadhi ya maovu yaliyofanywa na viongozi wa serikali na kuna baadhi ya hao waliotangaza nia walitetea maovu kwa nia ya kuisafisha serikali.

Sijapinga chama cha mapinduzi ila nafikiria hoja zao zisizo na uelekeo labda kama atakuja mwingine amabaye sijawahi kusikia maovu yake pamoja na majukumu yao! Sijui atakuwa Makamba? au atakuwa Membe? hapana huenda akawa Sitta sijui lakini.

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ni  safari iliyofika kikomo japo siajua kama watanzania wanamaisha bora mpaka sasa ila nimesikia elimu yetu imeshuka (haitamaniki), shilingi yetu haina maana tena labda ukienda Uganda ambako hawana viwanda kama taifa letu tajiri masikini kuliko.
Afya bado inasuasua lakini barabara zimejengwa sana kwa kiwango cha chini huku ajali zikiongezeka na kugharimu mamia ya watanzania.

Ngoja niende kwa jirani nikirudi wengine watakuwa wametangaza nia ila hawa wa leo ni LOWASSA,NCHEMBA,WASIRA,MWANDOSYA,SUMAYE,MAKONGORO ambao huenda wakapata nafasi ya kugombea nafasi ya urais kupitia chama chenye rangi ya kijani na njano.


(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

0 comments:

Post a Comment

 
Top