MANISPAA YA KINONDONI BADILISHENI MFUMO WA UPATIKANAJI WA LESENI

Wakati tunajisifu kuwa tupo katika karne ya sayansi na technolojia, ni muhimu kujisifu kuwa tunatumia sayansi na technolojia ili kurahisisha shughuli zetu za kila siku bila kupoteza muda wetu au wateja wetu tunaowahudumia.
Ni mabadiliko ya serikali yangu ya Tanzania ambayo mwaka jana imepata Rais ambaye anahimiza watu wake kufanya kazi kwa nguvu zote ili kukuza vipato vyao pamoja na serikali kupitia kodi inaotozwa na serikali hiyo makini kuwahi kutokea.
Kwa miaka mingi nchi imekuwa na tatizo kubwa la watu wake kutolipa kodi, lakini hali imebadilika katika kipindi cha serikali mpya ya Rais John Pombe Magufuli ambapo kila m tu anatakiwa kulipa ushuru kulingana na kipato chake.
Ni jambo zuri kila mtu alipe kodi kulingana na kipato chake , lakini ninaweza kusema kuna kodi utitili ambapo huenda mwananchi wa kipato cha chini ataathirika zaidi kuliko wale wenye biashara kubwa.
Kuna wakati nikajiuliuza, hivi serikali inataka watu wasifanye biashara au? Sikupata jibu kwa sababu kode imekuwa kubwa kiasi kwamba wafanyabiashara wanashindwa kupata faida katika biashara zao.
Hiyo sio lengo langu la kuuandikia umma wa wanatanzania kuhusu faida na hasara katika biashara zao kutokana na uwepo wa kodi utitili.
Napenda sana nilipe kodi ili Taifa langu lisonge mbele kiuchumi, pia napenda sana nikidhi vigezo vyote vya kufanya biashara hapa nchini lakini kuna shida moja ambayo kiukweli ikitatuliwa serikali itakuwa imetumia vizuri technolojia tuliyonayo na kurahisisha kazi kwa watumishi wake pamoja na walipa kodi(wafanyabiashara).
Kilio changu ni utaratibu unaotumiwa na serikali kutoa Leseni ya biashara pamoja na malipo yake, inatia kichefu chefu kiukweli mpaka najiuliza hivi mamlaka husika hamuoni hii hali? Bila shaka mmeona ila mmeamua kukaa kimya.
Mimi ni mkaazi wa Manispaa ya kinondoni wakati wa kutafuta Leseni yangu ya biashara imenichukua zaidi ya siku tano huku nikitumia siku nzima kukamilisha utaratibu wa kupata leseni yangu na bado sijaipata.
Fikiria kwa hizo siku tano nimepoteza kiasi gani? Mfano biashara yangu ninaweza kuuza 100000 kwa siku , maana yake kwa siku tano ni 500000 lakini wakati nafuatilia hiyo leseni sijauza kabisa. Hasara kwangu , hasara kwa serikali (call for change).
Hata hivyo kwa wale tuona-renew leseni utaambiwa ukalipie Bank ,ukirudi pale utaambiwa ukalete clearance form ya TRA , YES ni muhimu kuwa ni vitu vyote hivyo lakini kwanini tusiweke mamlaka zote sehemu moja ili kupunguza mzunguko kwa walipa kodi wenu?.
Nashauri Manispaa ya Kinondoni na nyingine ambazo zinazotumia mfumo kama huo kutumia mfumo wa kiasasa ambao utarahisisha kazi kwa watumishi wenu pamoja na walipa kodi wenu.
Badala ya kuwapangisha watu foleni na kujaza ofisi zenu kiasi cha watumishi kukosa hewa tumieni mfumo unaotumiwa na BRELA wa kujisajili kwa njia ya mtandao ambapo unafanya kila kitu ukiwa dukani , nyumbani au popote pale.
Huwezi kuamini saizi ukienda manispaa ya kinondoni kufuatilia leseni watu wamejaa utadhani kuna mkutano wa kisiasa , yaani ni zaidi ya kariakoo, hakuna njia ya kupita kabisa.
Kuna tabia ya serikali yangu inaposhauriwa au kukosolewa huwa inamchukulia mtu huyo kama mpinzani, kwa nia njema kabisa naomba badilisheni mfumo
 Amini nawambieni mtasifiwa endapo mtabadilisha mfumo mnaotumia sasa kwa sababu unapoteza muda na pia unakera walipa kodi.
Watu wanapojaa ofisin kwako si kwamba wewe ni mchapa kazi , ila kazi inakuchapa wewe kisha vilio vyako vitawakera unaowahudumia.
Badilikeni , tumieni mfumo wa kisasa kama wanaotumia wenzenu BRELA utawafaa .

Mpalamani Rockfeller
Grip & Lighting .



(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

0 comments:

Post a Comment

 
Top