kama hujui ulikotoka
huwezi kujua mahali ulipo wala sio rahisi kutambua wapi unaelekea japo
unaendelea kupiga hatua kuelekea usikokujua mwisho wa siku unajikuta umerudi
pale pale.
Ni wakati wa vipofu
kuona jua na viwete kutembea baada ya miaka 50 tangu wazaliwe na kufungiwa
ndani kama watu wasiojiweza wakati wengine wanamagari, majumba ya kisasa na
kufanya biashara kubwa hapa nchini.
Nikisema niwakati wa
mabadiliko halisi wapinga maendeleo watasema ujana unamsumbua na waliotufirisi
watasema anatuonea wivu kisa tuna pesa nyingi.
Mimi sio mwanasiasa
wala mwanaharakati kana kwamba natetea kambi rasmi inayolenga kulenga
mabadiliko ya kisiasa yatakayo badili mfumo mzima wa utawala, uchumi na jamii
kwa jumla bali mimi ni mtanzania niliyechoshwa na utawala usioonyesha njia ili
watu wake wasonge mbele.
Najisikia kichefuchefu
ila oktoba 25 lazima nikatapike kwa sababu wamewatesa wazee wetu bado
wanaendeleza mchezo wao mchafu wa kulifanya taifa hili la kwao na kutufanya
wengine wahamiaji tu.
Watanzania tusipoleta
mabadiliko mwaka huu ,tupelekwe India kwa matibabu ya akili maana hapa nyumbani
hatuna madaktari kisa watawala wanauwezo wa kuwafuata nje ya nchi. Aibu kubwa
japo wao wanafurahia tu.
Siasa inaendesha
uchumi ambao hujenga jamii bora ya kitanzania. Mfumo wa siasa ya Tanzania ni
duni hivyo tunahitaji mabadilko.
TASWIRA YA MABADILIKO KWA VIJANA.
Vijana wako mstari wa
mbele kuona kwamba taifa hili linakombolewa upya kutoka mikononi mwa waliopewa
uhuru 1961 ndio maana hawaoni uchungu wa kuiendeleza taifa lao kwa manufaa ya
watanzania wote.
Kazi kubwa imefanywa
na vijana waliopata nafasi ya kuingia katika vyombo vya maamuzi na kuongeza
uelewa wa kisiasa na utawala wa nchi hii kwa vijana wenzao.
Ni Dhahiri kwamba
vijana wakielimika ndio chachu ya mabadiliko kila sehemu haijalishi ni katika
hali gani (vijana ndio dira ya maendeleo).
Wenye upeo mdogo wa
kufikiri(samahani kwa neno hili kali) wanasema bado siasa ya nchi yetu inaenda
vizuri na taifa linakuwa kwa kasi sana, haina haja ya kubadili mfumo wa
kiutawala(I feel sorry if you are the one)
Lakini kuna vijana
wanaotaka kuwaonyesha watawala kuwa taifa hili ni la wote na halistahili kuwa
katika hali hii.
Lazima niwe wazi
katika hili , vijana wakitanzania wamehamasika na wameamka kushiriki katika siasa za nchi hii ,hapana
shaka mabadiliko yanakuja.
TASWIRA
YA MABADILIKO KWA WANAWAKE
Mwanamke anapenda
maendeleo ,hata katika nyumba mwanamke anapenda kununua vitu vyenye thamani na
vyenye kuvutia lakini ni muoga wa kufyeka njia itayoleta maendeleo.
Wakati mtazamo wa
vijana ni kubadili mfumo wa kisiasa hapa nchini wanawake wamekuwa nyuma kidogo
kutokana na hofu ya kuleta mabadiliko yatayoleta mageuzi ya kiuchumi wetu na
kijamii.
Wengine wanaona hakuna
sababu ya kuleta mabadiliko kwa sababu wanaona hata baada ya kubadili mfumo wa
utawala kazi yake ya kuoka mikate, mama ntilie itaendelea. Hivyo basi wanaona
kwa nini nipigane kuleta mabadiliko?(uelewa
mdogo wa siasa/political understanding is very limited most of the
women).
Wako wanawake wanaoona
kutaka mabadiliko katika taifa hili ni uhuni unaotaka kufanywa na vijana na
huenda kukatokea machafuko ambapo wanawake wanakuwa wahanga (fikra potofu). Lakini
hawaridhishwi ni mfumo uliopo.
Wengine wanasema
tukiwapigia kura wanaotaka mabadiliko watakuwa kama hawa hawa , kwa nini
nihangaike kuleta mabadiliko(kuishi kwa mazoea na kushindwa kufikiri maisha ya
badae).
Hapana shaka nikisema
naona Tanzania mpya inakuja ,kufikia hapa lazima niunge mkono mabadiliko.Hawa
watu wakibaki wataongea sana tena kwa dharau na kuendeleza ukandamizaji kwa
raia.
TASWIRA YA MABADILIKO
KWA WANAUME
Kwa asilimia kubwa
wanaume wanauelewa mkubwa wa siasa, lakini wamegawanyika katika makundi
mbalimbali kulingana na mahitaji ya mtu husika.
Wapo wanaume wenye
taswira waliyonayo wanawake kuhusu mabadiliko kutokana na kukosa elimu ya
kujitambua na uelewa mdogo wa siasa za nchi hii (Baadhi ya wanaume wamekosa
ujasiri kuleta mabadiliko na wengine wanaona maisha tunayoishi ni halali
yetu)…….badilika kabla ya octoba 25/be strong.
Lakini pia kuna
wanaume wanaofaidika na mfumo wa utawala uliopo, japo wanaona kuna kila dalili
na umuhimu wa kubadili mfumo, wao wameziba masikio kana kwamba hawasikii vilio
vya watanzania (conservative).
Kuna kundi kubwa la
wanaume kwa sasa linataka mabadiliko kwa sababu wengi wao wanateseka na
kunyanyaswa na mfumo huu usiofaa. Kuna makundi ya wakulima(ruzuku) ,
madereva(leseni), walimu(Mishahara), wafanyabiashara(EFD)….mabadiliko ni
lazima/change is inevitable.
MAAJABU YA TANZANIA
YANAYONIFANYA NIHITAJIA MABADILIKO.
-Tanzania ni nchi
pekee ambayo viongozi wanagawana pesa za umma na viongozi ngazi ya juu
wanacheka na wengine wasaidiana ili mwenzao asikamatwe (ujinga).
-Tanzania ni nchi
pekee ambayo 1.6Bil- ni pesa ya mboga na 400mil- ni vijisenti (dharau).
-Nchi ambayo wananunua
bidhaa lakini hawataki kurudishiwa chenji hadi mwenye duka akuletee(kutojali)
-Nchi yangu hupati
kazi bila kuwa na ndugu , rafiki au jamaa labda uwe mwalimu(umimi).
-Nchi ambayo mwalimu
wa primary ni yule aliyefeli form four
-Wanafunzi wanakaa
chini wakati kuna misitu kibao
-Nchi ambaye wananunua
ndege ambaye haiwezi kuruka na hakuna wa kuwajibika(wanahisi hatuelewi)
-Nchi ambayo mabasi
yanaletwa lakini milango iko kinyume na kituo na hakuna anaewajibika au
kuwajibishwa.(umakini)
-Nchi ambayo unaumwa
kichwa unapasuliwa goti(umakini) but who care?
-Nchi ambayo waleta
maendeleo wanafutwa katika ramani ya dunia.
-Nchi ambayo polisi
anajua haki za raia kuliko raia mwenyewe(elimu ya kujitambua hakuna).
-wanawake
wanajifungulia njiani hata akifikishwa zahanati hamna wahudumu wala vitanda vya
kulazwa, (nani akujali wakati wake zao wanajifungulia marekani).
Kwa kifupi hii ndio
nchi yangu ambayo kila kitu tunaletewa kutoka nje wakati tuna kila kitu
kinachoweza kutufanya tuwe watengenezaji wa bidhaa mbalimbali na kuziuza nje ya
nchi.
Utasema nini watu
wanafanya biashara ya malori wewe raia unataka reli ya kati itengenezwe? kama unadhani majangili ni raia wa kawaida
basi umenoa, kwa ulinzi na usalama wa nchi hii mtu angewekwa ndani kesi zingekuwa
on fire now.
TANESCO inakata umeme
wiki tatu ,nani anajali? Au nani amewajibika? Fimbo yako kura yako ,tuwachape
octoba 25(watanzania wanapoteza mamilioni ya pesa kutona na kukatika kwa umeme)
Maji hayatoki katika
nchi iliyobarikiwa mito ,maziwa na bahari(tuwaonyeshe octoba 25, binafsi
nimewachoka hawa wadudu).
Mpoto anasema
kukumbatia hewa kama mti ni ujinga, mimi nasema heri debe tupu kuliko sifuri.
Lakini maandiko yanasema mti usiozaa matunda ukatwe na uchomwe moto,Bwana
asema.
Wacha tuseme ukweli
hata Musa alikuwa anaishi Misri lakini aliwakomboa wanaisraeli japo hakufika
Kanani lakini Joshua aliwafikisha na wakawa huru.
TWENDE
TUKAPIGE KURA.
TIME FOR CHANGE,
NO MATTER WHAT!
0 comments:
Post a Comment